Mkuu Wa Mkoa Mjini Magharibi  Ayoub Mohammed Mahmoud  amewataka wanaochemsha na kuanika madagaa katika sehemu ya  Maruhubi kuhamia eneo lililotengwa na Serikali liliopo Kihinani ifikapo tarehe 21-9 2018 mwaka huu.

Hayo aliyasema leo huko  Maruhubi wakati alipokuwa   akizungumza na wajasiriamali wanaoanika madagaa   baada ya kukamilisha ziara  kukagua sehemu iliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo iliopo Kihinani .

Alisema anatarajia ifikapo muda huo wataanza shughuli zao kule walikotengewa na Serikali kwa lengo la kuepuka usumbufu , hivyo amewataka waanze kubomoa mabanda kwa utaratibu ili ikifika tarehe hiyo wawe washakamilisha zoezi hilo.

Aliwafahamisha wananchi hao kuondoka kwa usalama na waende wakafanye shughuli zao kama kawaida bila ya usumbufu wowote na kuwataka waendeleze sifa zao kama kawaida kwa kuendeleza amani na utulivu ndani ya sehemu hiyo mpya.

Pia aliwanasihi vijana wajiepushe kukaa maskani bila ya kazi maalum waendelee kujifanyia kazi zao kuanika madagaa na kujipatia kipato chao cha halali na kuepuka kujishirikisha na makundi maovu ambayo yatawapelekea kujiingiza katika uuzaji waunga au bangi na kuharibu mstakabali mzima wa maisha yao.

Vile vile amewaomba wale wote walioorodheshwa wapatiwe nafasi hizo kwa lengo la kuendeleza kazi zao kila mwenye haki ya kupatiwa sehemu kule apewe kwa kujifanyia shughuli zao  bila ya usumbufu wowote.

Nae Mwenyekiti wa ushirika wa kuanika madagaa Haji Omar Haji  amesema wapo tayari kuhamia katika sehemu waliyotengewa na Serikali bila ya matatizo yeyote ifikapo tarehe iliyowekwa  .

Aliomba wakati  vinapowekwa vikao kuhusu kuhama katika sehemu waliyokuweko hiv isasa nakuhamia waklikotengewa   na wao washirikishwe ili kwa lengo la kufikia maamuzi yaliyo sahihi.

Nao wananchi hao wamesema wako tayari kuhamia huko Kihinani Bububu walikotengewa  na Serikali ikiwa ni ahadi waliyoahidiwa na Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kuendeleza biashara yao hiyo  ya uanikaji wa madagaa.

Na Mwashungi Tahir.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed  Mahamoud akimsikiliza  Mwenyekilti wa Na Haji Omari Haji mpishi wa Biashara  ya Madagaa wakati alipofanya  ziara ya eneo la Bububu kihinani linalotarajiwa kauhamia hivi karibuni na kuondoka katika eneo la zamani lililopo  Maruhubi.

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed  Mahamoud  akiangalia Mchoro wa Ramani ya mabanda  ya wapika Madagaa yatakayojengwa katika eneo hili mara watakapohamia katika eneo hilo (kulia)   Khamis Hilika Khamis ni Msaidizi Afisa  ya Mipango Miji Manispaa ya Magharib “A” .

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed  Mahamoud akiangalia jinsi madagaa yanavyopikwa kwatumia kigamuzi wakatialipofanya zaiara katika eneo la Maruhubi.

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed  Mahamoud akitembelea eneo la wafanya biashara ya madagaa wakati alipofika katika eneo hilo.

Picha na Miza Othaman Maelezo Zanzibar.