Kamati Kuu ya CHADEMA imewavua uanachama na nafasi zote za uongozi wanachama 19 wa chama hicho walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum. Waliokumbwa na adhabu hiyo ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya na Esther Matiko.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakati akizungumaza na waandishi wa habari ameongteza kuwa

“wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa” Mbowe

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” Mbowe