Wakati Bunge la 11 likitarajiwa kumalizika Juni 19, mwaka huu, imeelezwa kuwa wabunge waliopanga katika nyumba za serikali mjini Dodoma, wameanza kupewa barua za kutakiwa kuondoka.

Mbunge wa Rufiji Mohammed Mcherengwa ,aliyasema hayo jana  Bungeni wakati akiomba muongozo wa spika kuhusu suala hilo, huku akimuomba spika Job Ndugai , kuzungumza na Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Isaack Kamwelwe , kuliangalia upya suala hilo na  kuwa na subira hadi uchunguzi utakapomalizika.