Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania wamejihakikishia kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10 kutoka kwa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na wachezaji hao juzi wakati Waziri Mkuu alipotembelea kambi yao, Makonda ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kamati yake itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Timu ya soka ya Taifa, Stars, imekuwa miongoni mwa timu nne zilizofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuifunga Uganda  ‘The Crane’ magoli matatu kwa sifuri.


Mechi hiyo dhidi ya Taifa Stars na Uganda the Craines imecheza katika Uwanja wa Taifa jana (Jumapili, Machi 24, 2019) ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwaongoza Watanzania kushuhudia mechi hiyo.


Taifa Stars imefuzu michuano hiyo itakayofanyika mwaka huu nchini Misri baada ya kupita miaka 39 tangu mara ya mwisho kucheza michuanohiyo.Timu hiyo kwa sasa imeungana na Burundi, Kenya na Uganda kufuzu michuano hiyo.