Jeshi la Polisi Kanda Maalum Tarime na Rorya limewafikisha mahakamani raia watatu wa wenye asili ya China, wakiwa na madini yenye uzito wa KG 300 ikiwemo dhahabu wakisafirisha kwenda nchi jirani.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi kilichofanywa na raia hao wa kigeni ni makosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania na kueleza wanachotuhumiwa ni kukutwa na madini bila ya kibali pamoja na kuhujumu uchumi.

Katika misako ya polisi kikosi cha usalama barabarani liliwanasa raia hao watatu  watatu wakiwa na gari aina ya TOYOTA Land Cruiser yenye namba za usajili wa Kenya KBW 515L.

Tulivyowakamata tulipeleka mawe waliyokuwa nayo kwa mtaalamu wa madini Dodoma, na alithibitisjha kuwa mawe yaliyokamatwa yalikuwa yana madini, na watuhumiwa wamefikishwa mahakamani kwa makosa 2 ya uhujumu uchumi na kukutwa na madini bila kibali” amesema RPC Henry Mwaibambe