Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiang’i ameagiza Raia wanne wa China waliokamatwa na Polisi kwa kosa la kumchapa viboko Mfanyakazi kurudishwa kwao

Agizo la Waziri linakuja siku chache baada ya Ou Qiang, Deng Hailan, Chang Yueping na Yu-Ling kukamatwa, kufuatia kusambaa kwa video iliyoonesha Simon Oseko ambaye ni Raia wa Kenya akichapwa viboko kwa kosa la kuchelewa kazini

Aidha, imeelezwa kuwa Wachina hao wamekuwa wakifanya kazi bila kuwa na Vibali

Hii sio mara ya kwanza kwa Kenya kurudisha Wachina nyumbani kwao. Wafanyabiashara saba walirudishwa China mwaka 2019 baada ya kukutwa na hatia ya kufanya biashara kinyume na Sheria