Wafanyabiashara wa vileo wapigwa marufuku Zanzibar

Wafanyabiashara ambao hawakuomba Vibali kwa mwaka huu 2019  vya kuuzia Vileo wametakiwa kuacha kuuza biashara hiyo kwa njia ya magendo kwani mahakama itawafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumza Nje ya Mahakama ya Mwanakwerekwe Katibu wa Mahakama hiyo Saleh Ali Abdalla amesema zipo baa wamiliki wake hawajaomba vibali kwa mwaka huu kwa ajili ya kufanyabiashara hiyo hivyo hawaruhusiwi kuuza vileo kwani hawajafata taratibu za uombaji kama walivyofanya wafanyabiashara wengine.

Amesema uuzaji wa vileo unasheria zake bila kibali na lessen ya kuuzia vitu hivyo lazima uchukuliwe hatua za kisheria kwani biashara yako haipo halali.

Hata hivyo Saleh amesema Mahakama  ya Vileo itakapo maliza utoaji wa maamuzi kwa baa zilizopata au kukosa bodi lazima itafanya ziara za kuzikagua baa zilizopewa vibali ili kuona utendaji wa kazi zao kama unaridhisha au laa! Nakama wakigundua ubabaifu basi watazichukulia hatua baa hizo.

Aidha amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yao ili kuhakikisha baa zilizofungiwa hazifanyi tena kazi kwa mwaka huu.


Amina Omar