Polisi mjini Garissa wameanzisha juhudi za kuwaokoa Abdulahi Isaack Harun na Abdi Hassan wanaoaminika kutekwa nyara jana Asubuhi na Wanachama wa Kundi la Al-Shabaab

Watu hao walikuwa wakisafirisha ‘Miraa’ kutoka Garissa kwenda Liboi, lakini walipofika Wardeglo Dam wakatekwa nyara na inashukiwa walipelekwa Somalia

Magari waliyokuwa nayo wafanyabiashara hao yalionekana mara ya mwisho eneo la Osman Baret kwenye mpaka wa Abdisugow na Gubahadhe mpakani Somalia

Hayo yanajiri wiki mbili tu baada ya Al-Shabaab kuteka nyara basi moja kutoka Garissa na kuwaua watu 10 wakiwemo maafisa wa polisi 6