Kikosi cha ulinzi ya mapinduzi cha Iran kimeikamata meli ya mafuta ya kigeni katika eneo la Ghuba na kuwakamata wafanyakazi wake 12, wakiwashutumu kwa kusafirisha mafuta kwa njia haramu, shirika la habari la Tasnim limeripoti

Meli hiyo ilikuwa imebeba lita milioni moja za mafuta wakati ilipokamatwa wakati ikipita katika ujia wa maji wa Hormuz , kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, ambalo halikusema ni taifa gani meli hiyo inatoka ama inatoa huduma kwa kampuni gani.

Eneo hilo la Ghuba ni moja kati ya maeneo muhimu ya njia za majini kwa ajili ya kusafirisha mafuta.

Eneo hilo limekuwa tete wakati hali ya wasi wasi ikiendelea kuongezeka kati ya Iran na Marekani kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayosambaratika na mataifa yenye nguvu duniani na hofu inaongezeka kuwa pande hizo mbili zinasogea karibu na makabiliano ya kijeshi.