Wamiliki wa akaunti 50 za Facebook zinazounga mkono chama tawala nchini Uganda cha National Resistance Movement [NRM] wamedai akaunti zao zilifungwa huku jumbe zao zikifutwa kabisa au kushidwa kuchapishwa kupitia mtandao huo wa kijamii.

Wafuasi hao wa rais Yoweri Museveni wamelalamikia kampuni ya Facebook kwa madai kuwa ilifunga akaunti zao kwenye mtandao huo.

“Aibu kwa mamlaka za kigeni ambazo zinadai zinaweza kupandikiza uongozi wanaoweza kuutumia kwa kuzuia utendaji wa akaunti za mtandao za wafuasi wa NRM . Hautamtoa RaisYoweri Kaguta Museveni,” alisema afisa wa habari wa rais Don Wanyama.