Wafungwa 180 kutoka Gereza lenye Ulinzi mkali la Shimo la Tewa lililopo Mombasa Nchin Kenya wametolewa na kutakiwa kukamilisha vifungo vyao nyumbani

Kutolewa kwa wafungwa hao ni mkakati wa Mahakama na Polisi katika kupunguza msongamano uliopo gerezani ili kuepusha maambukizi

Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya walioachiwa wametumikia robo tatu ya vifungo vyao na wametakiwa kumalizia adhabu zao nyumbani bila kufanya uhalifu wala makosa ya aina yoyote

Wafungwa hao watakuwa chini ya uangalizi na watapangiwa kufanya kazi za kijamii chini ya uangalizi wa Polisi, na wametakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi katika vituo ambavyo walikamatwa ndani ya saa 48 baada ya kuachiwa