Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu amethibitisha kuwepo kwa kesi mpya nne za maambukizi ya corona zilizopatikana DSM, Mwanza na Zanzibar na kufanya jumla ya kesi 24 zilizoripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huu Tanzania, wagonjwa hawa ni pamoja na wawili ambao wametolewa taarifa na Waziri wa Afya Zanzibar April 05, 2020.


“Wagonjwa wawili wapya wa corona Tanzania Bara ni Mwanaume(41) Raia wa Tanzania, mkazi wa Mwanza aliyeingia Tanzania kutoka Dubai kupitia uwanja wa ndege wa JNIA na kuelekea Mwanza na mwingine ni Mwanaume (35) Raia wa Tanzania, mkazi wa DSM, mfanyabiashara, wote wapi chini ya uangalizi wa watoa huduma” amesema waziri Ummy.