Wajumbe kamati za mashauriano Shehia na Mabaraza ya Wadi kushirikiana Zanzibar

Mkuu wa Wilaya Magharibi ( B ) Captain Silima Haji amewataka wajumbe wa Kamati za mashauriano za Shehia na Mabaraza ya Wadi kushirikiana ili kuimarisha umoja katika maeneo yao.

Ameyasema hayo  alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo  wajumbe  wa Kamati hizo katika Skuli ya Sekondari Mpendae .

Mkuu wa Wilaya Magharibi “B” Captein Silima Haji akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati za Mashauriano za shehia na Mabaraza ya wadi katika Skuli ya Sekondari ya Mpendae (kulia) Katibu Tawala Magharib “B” Hamza Ibrahim na Mstahiki Meya Manispaa Magharibi “B” Amour Ali Mussa.

Amesema katika  kuimarisha  umoja kwa wajumbe kutaweza kuibua matatizo mbalimbali na kuweza  kupelekea mabaraza hayo kusonga mbele kwa ajili ya  maendeleo ya wananchi .

Nae mwalimu  Hawa Said Kassim Afisa Mifugo Baraza La Manispaa Magharibi( B) amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa kwa wajumbe wa mabaraza ya wadi na kamati ya mashauriano za shehia jinsi ya kuibua miradi katika maeneo yao.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Mashauriano za Shehia za Magharibi B na Mabaraza ya Wadi wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya utekelezaji wa majukumu yao.

Alisema kuna  miradi miwili   ya Serikali na wananchi , ya Serikali hii ni mikubwa inayoratibiwa na Serikali kuu kama vile mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege , ujenzi wa barabara kuu ujenzi wa Nyumba za Maendeleo na  Usambazaji maji .

Mjumbe wa Baraza la Wadi ya Pangawe Mmanga Haji akitoa mchango wake juu ya mafunzo aliyopatia

Miradi ya wananchi kama vile ujenzi wa madrasa,  ukarabati wa njia korofi katika mitaa, utengenezaji wa sabuni na kazi za mikono ikiwemo  ufinyanzi.

Aidha alisema utekelezaji wa mradi huu unahusisha uwekezaji wa rasilimali mbali mbali zilizoainishwa kutumika ili kutoa matokeo yaliyo kusudiwa pia zina husisha kufanyika kwa kazi zote zilizoainishwa katika mpango kazi .

Pia  alisema  ili kufikia makubaliano ya pamoja katika uandaaji wa mradi ni muhimu paweze kuwa na ushirikiano na ushirikishwaji wa jamii husika .

Hata hivyo  alisema endapo kutaandaliwa mpango kuhusu mradi huu itapelekea kufikia malengo ya mradi huo na kupelekea maendeleo kwa wananchi .

Vile vile alisema viongozi wa mradi huo  wanapaswa kuhakikisha kuwa matatizo yanayo onekanwa kujitokeza yafanyiwe marekebisho  katika mabaraza hayo mapema .

 Fatma Makame     –    Maelezo  Zanzibar.