Wakati ‘ZAA’ ipo katika matayarisho ya kutoa wanariadha Gulam aja na ndoto zake

Wakati chama cha riadha Zanzibar (ZAA) kipo katika matayarisho ya kutoa wanariadha kutoka Zanzibar kuwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Onlimpiki 2020 nchini Japan.

Tumefanikiwa kuzungumza na Nguli na bingwa wa riadha za mbio fupi Tanzania na Zanzibari ambaye ameibuka kuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano yaliomalizika ya wilaya Ali Khamis Gulam amesema ndoto zake ni kuwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Onlimpiki huko japan 2020.

Aidha Gulam amesema kwa sasa wako katika mazoezi makubwa ya kujiandaa na mchujo wa mashindano hayo utakao fanyika Uganda ili kuweza kupata nafasi ya kuwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Onlimpiki kwenye mashindano ya mita mia mbili na mita mianne.

Kwa upande mwengine Gulama amekitaka chama cha riadha Zanzibar kuwafanyia mandalizi ya uhakika wanariadha wa Zanzibar ili kupata uwakilishi kwenye mashindano hayo makubwa ya dunia ikiwemo kupatiwa kambi za muda mrefu badala ya zile za muda mfupi.

’kule wezentu wamendelea sana mimi nilienda nchi za ulaya kwenye kozi za riadha za mazoezi wezentu wamejindaa vizuri wanafedha wanakuwa na kambi za muda mrefu bajeti zao zinakushawishi kufanya bidii ila sisi tunaweza ila mipango inahitajika tu’’ Alimalizia Ali Gulam.