Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Sheikh Abdallah Talib Abdallah amesema Maustadh na Waalimu wa vyuo vya Qur-an wametakiwa kuwashajihisha wafuasi wao kuanzisha elimu ya Maandalizi kwa watoto wao ili kutekeleza Sera ya elimu ya mwaka 2006.

Ameeleza hayo wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Walimu wa vyuo vya Qur-ani,kwenye  yaliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani Wilaya ya Mjini Unguja.

Amesema sera hiyo inataka kuanzishwa elimu ya maandalizi watoto waliofikia umri wa miaka 4 na elimu ya msingi kwa waliofikia umri wa miaka 6.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Safia Ali Rijali amesema wameamua kutoa mafunzo hayo ili kuhakikisha walimu wanapata mbinu bora za ufundishaji kwa wanafunzi wao na kuepukana na kusomesha kwa mazoea.

Hata hivyo ameuomba Uongozi wa Afisi ya Mufti Zanzibar kuweka Muongozo maalum utakaowawezesha waalimu hao kusomesha mtaala mmoja ili baadae waweze kutoa vyeti kwa walimu watakaohitimu.

Na: Takdiri Ali.