Walimu wa somo la Elimu ya michezo  (Physical Education) wamejumuika kwenye semina ya mafunzo ya michezo iliyohusisha walimu wa wilaya zote kutoka Unguja ya kupinga kampeni ya udhalilishaji wa watoto ambayo inaratibiwa na wakufunzi kutoka shirika la UNICEF kupitia “Coach Cross continet Country“ chini ya mradi wa “Micheal Josson Young Leader “ yenye lengo la kundoa udhalilishaji wa kingono .

Akizugumza na Zanzibar 24 Balozi wa mafunzo hayo kupitia mradi huo Fatma Ahmedi amesema mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha watotao wanakuwa salama kwenye maisha ya michezo ili kuondoa hofu kwa watoto hao.

Aidha alisema mafunzo hayo hufanyika kwa nchi 53 za Afrika ikiwemo zile nchi zilizoshamiri matukio ya udhalilishaji kwa watoto chini ya umri wa miaka 18 ili kuwapa motisha watoto kucheza michezo mbali mbali.

Alifafanua mafunzo hayo huwa ni vitendo na darasani ili kuwaelesha walimu hawa ambao ndio walezi wa watoto hivyo wanajukumu la kuwalinda ndio maana hupewa mafunzo ya kuwalinda watoto na udhalilishaji.

“Niliamua kuanzisha jambo ambalo lipo katika mazingira yangu nikiwa kama Balozi wa Micheal Jackson Young Leader ni kaona watoto wake wanakatazwa kushiriki michezo kwa kuhofia kunfanyiwa vitendo vibaya ,nkamua tuwape mafunzo walimu wa michezo na vilabu” Alifafanua Fatma Ahmedi.

Aidha amesema yeye binafsi amewafikia wanafunzi takribani mia moja ili kuonyesha watoto wanaweza kufanya michezo mbali mbali na kuondolewa hofu ya maisha yao na kujiona sehemu ya jamii.

“Mafunzo haya yanawajengea uwezo walimu hawa kuwa karibu na watoto na kujiona wao ni walezi wa wanafunzi baada ya wazee wao majumbani” Alimalizia Fatma.

Mafunzo hayo ya wiki moja  hufanyika Uwanja wa Amani Unguja yakihusisha walimu takribani 40 kutoka wilaya mbali mbli yanatarajia kumalizika wiki hii na kundelae kufanyika kisiwani Pemba wiki ijayo kwa walimu wa michezo wa wilaya zote za Pemba.