Walioibuka kidedea fainali ligi ya mpira wa mikono Zanzibar

Vijana visiwani Zanzibar wametakiwa kujiunga na michezo mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha afya zao sambamba na kujenga Umoja, Upendo na Ushirikiano baina yao na mataifa ya nje.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla Ali,  katika uwanja wa Nyuki Jeshini Unguja katika Fainali ya ligi ya Mpira wa Mikono Zanzibar.

Amesema endapo mchezo huo utatumika kikamilifu mafanikio yatapatika katika kuinua vipaji kwa vijana  kupitia mpira wa mikono Zanzibar .

Ameshauri mchezo huo kuwa endelevu kwa lengo la kutafuta vipaji kwa mafanikio ya vijana wa leo na baadae.

Aidha amezipongeza timu zilizoshiriki mashindano hayo pamoja na watendaji na kuaahidi kuwapatia timu moja kutoka katika kikosi chake ambacho kitashiriki ligi hiyo katika msimu unaokuja wa ligi kuu ya Zanzibar ya Mpira wa Mikono.

Bingwa wa fainali hiyo kwa upande wa wanawake Vijana ni timu ya Uzini na kwa upande wa wakubwa  timu ya JKU na makamu bingwa  ni Mwanakwerekwe Vijana na wakubwa ni  KMKM.

Na kwaupande wa wanaume bingwa ni timu ya Ndijani vijana  wakubwa ni  JKU na makamu bingwa ni Mwanakwerekwe vijana  na KMKM wakubwa.