Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza maambukizi mapya ambapo mgonjwa mmoja raia wa Marekani, Mwanamke (42) amethibitika Jijini Dar

Mgonjwa huyo amekuwa karibu na mtu aliyesafiri nje ya nchi na baadaye kuthibitika kuwa na maambukizi ya COVID19 aliporejea nchini

Aidha, ameeleza kuwa mmoja wa wagonjwa walio katika Kituo cha Temeke Jijini Dar, mnamo Machi 31 smethibitika kupona COVID19 na kufanya jumla ya waliopona kufikia wawili

Amemalizia kwa kusema kuwa jumla ya Wagonjwa 17 waliopo sasa wanaendelea kutibiwa na hali zao zinaendelea vizuri