Baraza La Manispaa Mjini Unguja Limewataka Wafanya Biashara Wadogo Wadogo Marufu Kama Wamachinga Kushirikiana Na Baraza Katika Kuweka Mji kuwa Safi Na Salama.

Wito Huo Umetolewa Na Mstahiki Meya Wa Baraza La Manispaa Mjini Unguja Khatib Abdurahman Khatib Wakati Alipokua Katika Ziara Ya Kukaguwa Wafanya Biashara Wadogo Wadogo Katika Eneo La Darajani Vikokotoni.

Meya Huyo Amewataka Wafanya Biashara Hao Wasifanye Biashara Katika Maeneo Ya Barabarani.

Nae Mkurugenzi Wa Baraza La Manispaa Ya Mjini Unguja  Said Juma Ahmada Amesema Lego La Baraza Ni Kuwaekea Mazingira Mazuri Wafanya Biashara Hao Na Wanatakiwa Kutowa Mashirikiano Na Baraza Pale Wanapo Hitajika.

Kwaupande Wao Wafanya Biashara Hao Mussa Omar  Na Gress Makungu  Wameliomba Baraza Kuwawekea Utaratibu Nzuri Katika Maeneo Wanayo Fanyia Biashara Zao ili kuwepuka usumbufu unao jitokeza.