Wanafunzi  wanaomaliza  elimu ya juu nchini  wametakiwa kubadili fikra zao za kusubiri  ajira serikalini na badala yake wajijengee uwezo  wa kujiajiri wenyewe kwa  kujishughulisha na kazi za ujasiriamali.

Akizungumza na Zenji fm Katibu wa Jumuiya ya kupambana na changamoto zinazowakabili  Vijana ZAFAYCO Abdalla Ali Abeid  na Katibu wa Jumuiya ya Zanzibar Youth Forum Almas Mohammed wamesema kutokana na ongezeko kubwa la vijana waliomaliza vyuo ambao hawana ajira  ni vyema vijana  wakabadili  mitazamo yao ya kusubiri ajira serikalini  na badala yake  watafute mbinu mbadala itakayowawezesha kuwainua kiuchumi.

Hata hivyo wamesema kutokana na vijana wengi  bado hawana taaluma ya ujasiriamali  serikali inajukumu kubwa la kubadilisha mitaala ya kufundishia mashuleni kutoka katika  nadharia na badala yake iwe ya vitendo  ili kuwajenga vijana tokea mashuleni ili watakapo maliza watoke wakiwa na ujunzi utakaowasaidia  kubuni  mbinu mbadala ya kuwainua.

Aidha wamesema  hivi sasa Jumuiya zimekuwa na muamko wa kutosha wa kuwawezesha  vijana kuhakikisha  wanainuka kiuchumi  kwani  tafiti zinaonesha kuwa chanzo cha vijana kujiingiza katika makundi hatarishi  ya madawa ya kulevya  ni ukosefu wa ajira hivyo , serikali lazima iwajengee mazingira bora vijana kwani wao ndio   uti wa mgongo wa taifa kiuchumi.

Na:Amina Omar Zanzibar24