Wanafunzi watatu wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa jengo moja kati ya madarasa ya shule ya Msingi Bwawani, ambapo katika hao waliojeruhiwa wengine ni wanafunzi wa shule ya Msingi Kijichi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi wa Temeke, Andrew Masatya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema taarifa hizo amezipata muda si mrefu na ametuma timu ya kufuatilia zaidi tukio hilo.

”Ni kweli wanafunzi wa Bwawani wameangukiwa na Ukuta asubuhi hii, nimetuma timu yangu kwaajili ya uchunguzi zaidi, kuhusu idadi ya majeruhi maana nimeambiwa hakuna kifo lakini tayari baadhi ya majeruhi wameshafikishwa hospitali ya Wilaya kwaajili kupata huduma”, amesema Masatya.

Hata hivyo ripoti za awali zinaeleza kuwa mwanafunzi mmoja amefariki katika hao watatu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya kuangukiwa na ukuta.

Habari zaidi tutaendelea kukufahamisha baada ya uchunguzi wa polisi na ripoti ya madaktari.