Wanajeshi wa Mali wameuawa baada ya kushambuliwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa Magaidi, Mashariki mwa Nchi hiyo katika eneo la karibu na mpaka na Niger

Askari 24 wa Vikosi vya Mali na Magaidi 17 wameuawa katika mapigano hayo huku ikielezwa kuwa vifaa vingi vya wanamgambo hao vimeharibiwa vibaya

Wanajeshi wa Mali na Niger walikuwa wakifanya operesheni ya pamoja inayoitwa ‘Tongo Tongo’ katika eneo la karibu na mpaka unaozitenganisha nchi hizo mbili

Washambuliaji walikuwa kwenye gari 7 na pikipiki zikiwamo pikipiki za matairi matatu, ambazo ni mali ya kituo kimoja cha afya