Wananchi wa Ndunduke watakiwa kutunza sehemu za ibada

Wananchi wa kijiji cha Ndunduke Mkoa wa Magharibi “A” wametakiwa kuutunza msikiti mpya waliojengewa ili kuweza kurithiwa na vizazi hadi vizazi kwenye kijiji hicho.

Mskiti mpya uliojengwa na Shirika la Direct Aid kijiji cha  Ndunduke.

Akizugumza kwenye ufunguzi wa msikiti huo uliojengwa na Shirika la Direct Aid Katibu wa Ofisi ya Mufti Zanzibar Shekhe Fadhil Soraga amesema msikiti huo ni mali ya watu wa Ndunduke hivyo hakuna budi kuutunza na kuwa ni kituo cha elimu ya dini ndani ya kijiji hicho.

Aidha Fadhil Soraga amewapongeza Shirika la Direct Aid kwa kujikita katika kusaidia jamii ya Zanzibar ambayo imekuwa na changamoto kubwa katika kupiga hatua ya maendeleo na hata kijiji cha ndunduke kimeanza kufaidika na miradi ya shirika hilo la Direct Aid.

‘’Nilamfata mwenyewe mkuregenzi Shekhe Aiman kamal Din ofisini kwake kwerekwe ni kamueleza changamoto za watu wangu wa kijiji change cha ndunduke ya msikiti akanambia ntakujengea leo ameujenga bila ya shaka ndo tunaowana’’ Alisema Shekhe Fadhil Soraga.

Akizugumza kwa niaba ya Ofisi kuu ya shirika hilo Raisi wa kanda ya kusini wa Shirika hilo la Direct Aid Swalehe Ibrahim amesema shirika hilo limekuwa likifadhili miradi mbali mbali ya kijamii ikiwemo ujenzi wa maskuli,madrasa na huduma za maji.

Amesema ni jambo la kheri watu wanatumia fedha zao kuhakikisha wanasaidia jamii ya Zanzibar watu ambao Zanzibar hawajawahi kufika tangu kuanza kutumia fedha zao pasina kuwataka kuombea duwa ili kuweza kuwakomboa zaidi.

Nae mkuregenzi wa Shirika hilo kwa ofisi ya Zanzibar Aiman Mohamed Kamal Din amesema msikiti huo umechukua miezi minne kukamilika na jumla TSH Millioni Hamsini zimetumika kujenga msikiti huo .

Kwa niaba ya kijiji hicho mzee wa kijiji hicho Ali Zaidi Ali amesema wao wamepokea msikiti huo kwa mikono miwili na kupeleka shukrani zao kwa wote waliojitokeza kusaidia msikiti huo ikiwemo Ofisi ya Mufti na wadhamini wa kuu Shirika la Direct Aid.