Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Moudlin Cyrus Castico amewataka wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kuyaenzi mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 kwa kuunga mkono juhudi za Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Amesema Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatumia fedha nyingi kuhakikisha kero zinazo wasumbua wananchi zinapatiwa ufumbuzi kama alama tosha ya kudumisha na kuyaenzi mapinduzi hayo kwa vitendo.

Mh Castico ameyasema hayo huko kifundi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akifungua mradi wa maji safi na salama utakao wanufaisha wananchi wa kifundi na mgogoni ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 54 ya mapinduzi  zanzibar.

Amefahamisha kuwa mpango wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar nikuhakikisha ifikapo mwaka 2020 nikuona wananchi  wa visiwani wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia %100 na kuwa hivi sasa ni shehia chache ambazo hazijanufaika na huduma hiyo.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman amewatanabahisha wananchi kuacha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto nakuwa  imeundwa  kamati maalum ili kukabiliana nahali hiyo.

Nae Afisa mdhamin Wizara ya Maji Nishati na Ardhi Nd. Juma Bakar Alawi amesema kuwa zaidi ya Tsh 67 Milioni zimetumika katika mradi huwo nakuwataka wananchi kulipia huduma hiyo kwa wakati nakuheshimu miundo mbinu hiyo kwa faida yao.