Wananchi watoa malalamiko ongezeko la nauli kiholela Unguja

Wananchi wanalalamikia ongezeko  la nauli kiholela kwa baadhi ya magari ya shamba yanayokwenda Nungwi,Chwaka pamoja na Dunga ambapo hata Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar haikupandisha nauli yoyote.

Akizungumza na zanzibar24 Mkuu wa Idara ya Usafiri na Leseni  Suleiman Kinoo Kirobo amesema kupitia tamko lao amewataka wananchi kutoa taarifa katika kituo cha polisi pamoja na kufika katika idara yao ya usafiri na leseni kuwapatia taarifa zao zinazohusu upandishaji nauli hizo kwani hilo ni kosa la jinai.

Nao Makamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja na Kaskazini Unguja  Makamishna Wasaidizi Wandamizi Suleiman Hassan Suleiman  na Haji Abdalla Haji wamesema kuwa hawajapata taarifa zozote zinazohusu kupandishwa kwa nauli kwa abiria  na kuwataka kuchukua namba za gari pamoja na eneo inayokwenda gari hiyo  ili kuweza kuchukuliwa hatua  za kisheria zidi ya wanaofanya makosa hayo.

Sambamba na hayo Abiria hao  wametakiwa kuripoti katika vituo vya polisi vilivyokaribu  na wao ilikuweza kutoa taarifa zao  na kufanyiwa kazi ipasavyo ilikuwepusha usumbufu unaojitokeza katika usafiri wao .

 Rauhiya mussa shaaban