Mwanasiasa wa upinzani kutoka nchini Rwanda Seif Bamporiki ambae alijifichamafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Ripoti zinasema Bamporiki aliuawa alipokuwa akiwasilisha samani kwa mteja Jumapili mchana mjini Cape Town Afrika Kusini.

Mpaka sasa bado haijabainika kama kifo chake kilichochewa na masuala ya kisiasa au vinginevyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mazingira ya kifo chake, waliomvamia walichukua simu zake za rununu na waleti kabla ya kuondoka eneo la tukio.

Bw. Bamporiki alikuwa mshirikishi wa chama cha Rwanda National Congress.

Story kwa msaada wa mtandao.