Watu 10 wamekamatwa na polisi Zanzibar kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Shirika la kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International limeripoti kuwa wanaume hao 10 wamekamatwa Jumamosi iliyopita katika fukwe ya Pongwe walipokuwa katika harusi ya mashoga. Wengine sita walifanikiwa kuwatoroka polisi.

“Polisi walifika eneo la tukio baada kupewa taarifa na wananchi kuwa kuna harusi ya mashoga inaendelea…Watu hao wanashikiliwa katika kituo cha polisi Chwaka na mpaka sasa hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa,” inasema ripoti ya Amnesty.

Sababu hawajakamatwa wakiwa wanafanya ngono, Naibu Mkurugenzi wa Amnesty kwa kanda ya Afrika Mashariki Seif Magongo anahofu kuwa watalazimishwa kufanyiwa vipimo.

Chanzo BB