Mastaa kadhaa wemetumia kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram kuonyesha hisia zao baada ya hukumu kutolewa ya kwenda jela miaka miwili kwa muigizaji wa filamu nchini, Elzabeth Michael ‘Lulu’ ambaye amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba.

Kufuatia hukumu hiyo mastaa wa muzuki na filamu pamoja na watu maarufu kama Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Shetta, Mwanasheria Albert Msando na wengineo wametumia kurasa hizo kuelezea hisia zao baada ya hukumu huku wengi wao wakionyesha kumpa moyo mrembo huyo.