Wasanii waanza kunyoosheana vidole sakata la mashoga

Ikiwa vuguvugu la oparesheni ya tokomeza mashoga ikiendelea jijini Dar es salaam, watanzania wameonekana kuhamishia vita hiyo pia nchini Nigeria, baada ya msanii Spice ambaye ana mahusiano na Lady Jaydee, kupiga picha na shoga maarufu nchini Nigeria, anayejulikana kwa jina la Bobrisky.

Balaa hilo limemkumba Spice baada ya kuchapisha picha katika mtandao wa Instagram akiwa na Bobrisky, na watanzania wakimkosoa kuwa hakupaswa kupiga picha na shoga huyo, huku wengine wakimtuhumu kuwa na yeye anajihusisha na vitendo hivyo.

Baada ya kuona mashambulizi yanazidi Spice aliamua kuwajibu Watanzania kwenye mtandao akisema kwamba “Nashangazwa na hili, hii ni ‘video shoot’ tu, hawa watu wapo hapa kunidhalilisha, hata komando wenu ananiita mimi shoga, fikiria, nimechukizwa sana”.

Hata hivyo baada ya ripota wetu kushtushwa na jibu hilo la Spice, akaingia kwenye ukurasa wake wa instagram na kukuta picha zote za Lady Jaydee zikiwa zimefutwa, hata zile za promo ya show ya Jaydee ya vocals night nazo zimefutwa.

Ikumbukwe tu hivi karibuni kulikuwa na tetesi za wawili hao kuachana, kwani ni muda mrefu umepita bila kuonekana wakiwa pamoja, jambo ambalo si kawaida yao.

Chanzo: Muungwana.