ACP Azizi Juma Mohammed  ambae pia aliwahi kua Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja (RPC) wa mkoa wa mjini magaribi alizaliwa tarehe 7/3 mwaka 1960 kijijini kwao Michakaeni Chake Chake Pemba.

Ambapo alipata elimu msingi na Sekondari katika shule ya Madungu mwaka 1977, ambapo Mwaka 1978 alikamilisha elimu yake ya sekondari katika shule  Feedelcastroo wilaya ya Chake Chake mkoa wa kusini Pemba.

Mwaaka 1979 alipata cheti cha Sheria katika chuo kikuu cha Dar er-salam ambapo mwaka 2016 alimaliza elimu ya Diploma ya usalama katika chuo cha ulinzi cha taifa kilichopo Dar-er-salam.

Mwaka 2002 Marehemu alishiriki mafunzo ya makosa ya jinai katika chuo cha Almubaraak nchini Misri.

Pamojana na mambo mengine wakati wa uhai wake Marehemu aliwahi kufanya kazi katika Maeneo mbalimbali ya Tanzania na kuwahi kuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Ambapo Hadi mauti yanamkuta Marehemu alikuwa mkuu wa kamati ya mapambo na sherehe za kitaifa katika jeshi la polisi Tanzania na ameacha vizuka wawili pamoja na watoto watano.