Mkuu wa dawati la jinsia na watoto la Tunguu Ali Mohammed Othman amewataka wazazi, walezi pamoja na walimu kuhakikisha wanarudi kwenye muongozo wa Dini zao ili kupunguza au kuondoa kabisa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia .

Akifungua mafunzo ya elimu ya udhalilishaji wa kijinsia katika skuli ya Mchangani wilaya ya kati Unguja ikiwa na lengo la kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia Mkuu huyo amesema ni vyema kwa wazazi, walezi pamoja na walimu kujuwa majukumu yao kwa watoto na kuwatengenezea pencheni ya baadae kutoka kwa watoto wao.

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto la Tunguu Ali Mohammed Othman akizungumza katika mafunzo ya elimu ya udhalilishaji wa kijinsia katika skuli ya Mchangani wilaya ya kati

Akizungumzia kuhusiana na suala la mada ya ukatili Shuwekha Zubeir amewataka watoto kutoa taarifa kwa wazazi  pindi pale wanapoona wanafanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na kuacha kuficha vitendo hivyo vinavyoharibu nguvu kazi ya taifa.

Aidha Mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto Bi. Khadija Haji ametoa tahadhari kwa wazazi na kuwataka kuwalinda watoto wao kutokana na vitendo hivyo vya Udhalishaji wa kijinsia vinavyotokea katika maeneo mbali mbali huku akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi dhidi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Nao wazazi pamoja na walezi wamewaomba dawati la jinsia na watoto kuwafanyia uchunguzi watoto katika skuli  ilikuona kama kwamba kuna kitendo chochote walichofanyiwa.

Ziara hiyo ya mafunzo ya Elimu ya udhalilishaji wa kijinsia iliandaliwa na dawati la kijinsia na watoto Tunguu limejadili mada mbili ikiwemo Udhalilishaji wa kijinsia pamoja na Ukatili

Hizi hapa ni picha mbalimbali katika mafunzo hayo

Rauhiya Mussa Shaaban