Serikali ya Tanzania imewarejesha nchini Watanzania 119 ambao walikwama Dubai kufuatia kuzuiwa kwa safari za ndege kutokana na mlipuko wa corona.

Ndege ya Fly Dubai imewarejesha Watanzania hao waliokuwa wamekwama Abu Dhabi na Dubai tangu March 25, 2020 Serikali ya Falme za Kiarabu ilipotoa zuio la kuingia na kutoka kwa ndege.