Pemba: Polisi yawashikilia watatu kwa kumuingilia mlemavu kinyme na maumbile

Jeshi la Polisi Kaskazini Pemba limewashikilia Vijana watatu wakaazi wa Pandani  Wete kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenzao ambaye ni mlemavu wa akili na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.

Tukio hilo limetokea tarehe 4/10/2018 majira ya saa 12 jioni huko Pandani ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kumuhadaa kisha kumchukua na kumfanyia kitendo cha liwati.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi kaskazini Pemba Shehan Mohd Shehan amesema, kati ya watu watatu wanaowashikilia kwa tuhuma ya kosa hilo wawili kati yao ni wadogo kisheria (wanamiaka kati ya 16 na 17) ambao wapo nje kwa dhamana na mmoja aliyetambulika kwa jina la Issa Sharif mweye umri wa zaidi ya miaka 32 bado wanaendelea kumshikilia kituoni hapo kwa mahojiano zaidi.

“hawakumbaka wala hawakumkamata kwa nguvu  ila walimchukua hadi porini kisha wakamfanyia hicho kitendo” alisema kamanda

Katika hatua nyengine kamanda Shehan amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi na utakapokamilika hawatosita kuipeleka mahakani kesi hiyo ili kwenda kujibu mashtaka yao.

Chanzo: pembatoday