Maeneo ya Somaliland na Puntland yakiathiriwa vibaya zaidi na mvua za msimu maarufu kama Deyr ambazo hunyesha Oktoba hadi Disemba, hazikunyesha kama ilivyotarajiwa mwaka uliopita wa 2018 na hivyo maeneo mengi Somalia sasa yanashuhudia kiangazi. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) watu milioni 4.9 kote Somalia wanahitaji misaada ya chakula huku watoto milioni 1.2 wakiwa wanakumbwa na tatizo la lishe duni.

Huku hayo yakijiri idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya imeeleza kuwa kimbunga cha idai katika Bahari ya Hindi ndicho kimechangia pakubwa ukosefu wa mvua katika maeneo mengi nchini humo

Naibu mkurugenzi wa idara hiyo Ayub Shaka anasema hali ya kiangazi katika maeneo mengi ya Kenya inatarajiwa kuendelea pamoja na kwua mvua zimeshuhudiwa katika baadhi ya maeneo. Hali sawa na hiyo inaripotiwa katika nchi za ukanda wa Pembe