Watu 10 walioripotiwa kufukiwa na kifusi cha mchanga usiku wa kuamkia leo Septemba 10, 2019 wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Tayari watu 8 wameokolewa wakiwa wazima huku mmoja akiaga dunia na mwingine akikwama mgodini.

Akithibisha taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,  Muliro Jumanne Muliro amesema ajali hiyo imetokea katika machimbo ya Shilalo katika Kata ya Inonelwa.

Kamanda Muliro, amesema polisi wamefanikiwa kuwaokoa watu 8 wakiwa wazima na huku mmoja wa 9 akiwa tayari amefariki dunia.

Muliro amesema mtu wa 10 aliyekwama juhudi za uokoaji bado zinaendelea ili kunusuru maisha yake.