Takriban watu 11 wameuawa baada ya watu wenye silaha kuvamia baa moja na kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwemo ndani ya baa hiyo iliyopo katika jimbo la kaskazini mwa Brazil la Para.

Msemaji wa jimbo hilo Natalia Mello amesema washambuliaji hao waliokuja wakiwa kwenye magari na pikipiki waliwashambulia watu hao kabla ya kukimbia.

Mello amesema vifo hivyo vilihusisha wanawake sita na wanaume watano, Kulingana na tovuti ya habari ya G1 polisi wamesema washambuliaji hao walikuwa 7, na mmoja alijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.