Miili 12 imepatikana katika eneo ulipotokea mlipuko wa bomba la mafuta katika kiwanda cha mafuta kilichoko Komkom, eneo la Oyigbo kwenye jimbo la Rivers lenye utajiri mkubwa wa mafuta nchini Nigeria.

Mwenyekiti wa serikali ya mitaa ya Oyigbo Bw. Gerald Oforji amesema miili hiyo imepatikana baada ya moto mkubwa kuzimwa.

Polisi wamesema haiwezekani kutambua idadi kamili ya watu waliofariki kwa sasa mpaka uchunguzi utakapokamilika. Pia wamesema haijulikani mmiliki wa kiwanda hicho.

Wakati huo huo, Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameeleza kusikitishwa na tukio hilo, na kuamuru uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ufanyike.