Hadi sasa watu 1,901 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Dengue nchini huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ukiwa na wagonjwa 1800, maambukizi yanaelezwa kupanda kwa kasi hadi watu 74 kwa siku kutoka watu 32.

Hayo yameelewa na mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari Kambi, amesema wagonjwa 1,901 wamethibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Dengue, na wengine tayari wamepona na wengine bado wanatibiwa katika hospitali na vituo vya afya nchini.