Takriban watu 22 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea jana katika barabara ya Batie-Baham, mkoa wa Magharibi nchini Cameroon.

Ajali hiyo ilitokea baada ya basi moja walilokuwa wakisafiria kuteleza na kugongana na lori uso kwa uso. Watu 19 walifariki papo hapo na wengine watatu walifariki hospitali.

Polisi wanasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwani bado kuna maiti nyingine ziko chini ya basi hilo linaloharibika vibaya