Takriban watu 22 wameuawa baada ya mapigano ya jamii juu ya wizi wa mifugo kati ya mikoa miwili ya kaskazini mwa Sudan Kusini.

Waziri wa Habari katika mkoa wa Twic unaozunguka kanda ya Kaskazini ya Liech, Michael Mayout aliliambia Shirika la habari la China Xinhua  kwamba mapigano hayo yaliyozuka siku ya Jumanne kati ya vijana kutoka maeneo mawili juu ya wizi wa mifugo pia yalisababisha kifo cha askari mmoja na kuwajeruhi watu wengine 18.

Mapigano ya jamii ya Sudan Kusini ambayo mara nyingi huhusisha wizi wa mifugo, kutekwa nyara kwa watoto na wanawake yamekuwa yakisababisha vifo vya maelfu ya watu nchini kote.