p

Watu 60 wamefariki kutokana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha maeneo ya kaskazini magharibi mwa Pakistan, maafisa wanasema.

Mvua kubwa ilianza kunyesha Jumamosi na kusababisha mafuruiko mikoa ya Khyber Pakhtunkhwa, Kashmir na Gilgit Baltistan.

Ingawa msimu wa mvua za pepo za msimu haujaanza, mvua za kabla ya msimu mara nyingi husababisha uharibifu hasa maeneo ya mashambani Pakistan ambapo miundo mbinu ni duni.

Maafisa wamesema wakazi wametakiwa waondoke na kukimbilia nyanda za juu na maeneo yaliyo salama.

Mwaka uliopita, zaidi ya watu 170 waliuawa wakati wa msimu wa mvua za masika nchini Pakistan.