Mratibu wa Mamlaka ya Taifa ya Kushughulikia Majanga ya Dharura, Ibrahim Farinloye amesema hadi kufikia jana usiku walikuwa wamepata miili ya watu 9 waliofariki.

Hadi sasa Watu 40 wameokolewa kutoka kwenye kifusi, wengine wakiwa na majeraha mabaya na bado watu wapatao 100 wanahofiwa kufunikwa na kifusi baada ya jengo hilo la ghorofa 3 kuanguka.

Wakazi wa maeneo ya jirani wanasema Watoto takribani 100 walihudhuria katika shule hiyo iliyokuwepo ghorofa ya juu kabisa kwenye jengo hilo lililokuwa na Ofisi, Maduka na Makazi ya Watu.

Hata hivyo, sababu ya jengo hilo lililokuwa eneo la Itafaji karibu na Soko kwenye mji wa Kibiashara wa Lagos kuanguka bado hazijafahamika