Zaidi ya watu nusu milioni wamefariki dunia kutokana na janga la virusi vya corona huku maambukizo duniani kote yakipindukia milioni 10

Takwimu hizo zimetolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Marekani imesalia kuwa nchi iliyo na maambukizo ya juu, ikiwa na vifo 125,000 na watu milioni mbili na nusu wameambukizwa maradhi hayo.

Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa kimesema visa vya maambukizi ya COVID-19 vimeongezeka barani Afrika katika kiwango kipya cha zaidi ya watu laki 371,000 ikiwemo vifo 9,484.

China imeweka vizuizi katika miji iliyo na wakaazi laki tano katika maeneo yanayozunguka mji wa Beijing ili kuzuia wimbi jipya la maambukizo, huku mamlaka zikionya kuwa mripuko huo bado ni mkubwa na mgumu.

chanzo:DW