Watu wawili wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na Fisi ambao hawakujulikana idadi yao, Baada ya kuvamia nyumba iliyokuwa na msiba katika kijiji cha Kasabunga wilayani Bunda mkoani Mara.

Image result for fisi kuvamia watu

Kwa mujibu wa Daktari wa Hospitali ya Misheni Kibara Dkt Samwel Paul, Ambako majeruhi hao wamelazwa, Alithibitisha kupokea majeruhi hao ambao walikuwa wamejeruhiwa sehemu mbalimbali kwenye miili yao ikiwemo kwenye mikono.

Majeruhi hao ni David Robert na Bi. Elizabeth Mgeta (60) wote walikuwa waombolezaji kwenye msiba huo.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo limetokea saa 6 usiku wa kuamkia jana, Ambapo waombolezaji walikuwa wanajiandaa kulala baada ya kumaliza mazishi.