Waumini wa Dini ya Kiislamu kote nchini wametakiwa kuzidisha Upendo, kusaidiana na kuhurumiana katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuweza kupata fadhila zinazotokana na mwezi huo.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Maalim wakati alipokuwa akizungumza na ZBC kuhusiana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaoendelea.

Amesema Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kuchuma mambo mema kama vile kuzidisha Kusoma Qur-an,Tas-bih na Swala za Usiku hivyo ni vyema kuzidisha Ibada ili kupata ujira mkubwa zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Aidha amewaasa Waumini hao kuwa Wazalendo wa nchi yao kwa kufuata misingi ya Dini inayosisitiza suala la  Amani na Utulivu.

Mbali na hayo amekemea baadhi ya Watu wanaofanya matendo mavu yaliokatazwa hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama vile kuvaa nguo zisizokuwa na stara kuacha mara moja ili kunusuru nmgogoro unaoweza kujitokeza.

Hata hivyo amewataka waumini wa Dini nyengine kutii sheria za nchi kwa kuepuka kuwafanyia vitendo vya kukihirisha ili kuepukana na migogoro inayoweza kuepukika.