Wavuvi 16 raia wa Tanzania wakamatwa nchini kenya

Mamlaka ya nchi ya Kenya zimewakamata Wavuvi 16 raia wa Tanzania kwa tuhuma za kuvuka mpaka na kutumia vifaa haramu vya uvuvi.

Watanzania hao wamekamatwa katika ufukwe wa Ziwa Victoria karibu na pwani ya Bamgot iliyopo ndani ya Kaunti ya Migori.

Waliwekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Macalder huku boti zao zikisalia katika pwani ya Bamgot. Mkuu wa Polisi wa eneo hilo amesema Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani baada ya mahojiano.

Katika kipindi kilichopita Wavuvi wa Kenya walikamatwa na Mamlaka za Tanzania na Uganda kwa makosa ya kuvuka mpaka.

Huku tukio la karibuni likiwa ni lile la Serikali ya Tanzania kuwakamata Wavuvi 36 wa Kenya kwa kuvuka mpaka wa bahari na kuingia kufanya shughuli za uvuvi nchini.