Kila ifikapo April 7 kila mwaka ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha jemedari na muasisi wa mapinduzi matukufu yaliyofanyika mwaka 1964 hayati Abeid Amani karume ambae alifariki kwa dhulma za wahaini.

Ni mwka wa 48 sasa toka tumpoteze jemedari huyu, Wazanzibar wataendelea kumkumbuka kwa yale mengi mazuri aliyoyotuachia na aliyoyafanya wakati wa uongozi wake ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata elimu bure, matababu bure, na kumpa kila mwananchi heka tatu, pia alijenga nyumba za makazi katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba zikiwemo zile nyumba maarufu za Michenzani pamoja na nyumba wazee katika maeneno ya Unguja na Pemba, huduma ya maji safi mjini na vijijini.

Hayati Abeid Amani Karume aliuwawa kwa kupigwa risasa na wapinga maendeleo. Hayati Karume amekufa kiwiliwili, mawazo, fikra na hekima zake bado zipo ambapo viongozi waliopo wanaendelea kuendeleza kwa vitendo.

Huyu ndie Hayati Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar na muasisi wa mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Jaunari 12, 1964. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi (Amiiin).