Mbunge wa Konde Pemba, Khatib Said Haji ametaja waziri aliyekataa kukaa karantini na kutoa wito kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumchukulia hatua kwani alionekana na dalili za ugonjwa wa Virusi vya Corona hali iliyohatarisha maisha ya watu wengine.

Hayo ameyabainisha jana Bungeni Dodoma wakati wa Mkutano wa 19, kikao cha tano cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mbunge huyu alisema

“Kuna mchezo, mzaha na dharau juu ya maisha ya watu wa Zanzibar juu ya ugonjwa huu wa Corona, Kuna Waziri mmoja alikuwa safari ya nje aliporudi Zanzibar katika hali ya kuumwa akakataa kukaa karantini, Waziri huyu Salama Aboud Talib alienda kukaa nyumbani kwake, alipozidiwa alirudi hospitali ya Mnazi Mmoja ndani ya muda wa siku 3 aling’ang’ania” 

Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema, “Alipotolewa kwa nguvu ndiyo akakubali kuwekwa karantini athari yake sasa nyumbani kwake kaambukiza watatu, hospital ya Mnazi Mmoja hatujui, je kiburi hiki kakitoa wapi?, sasa ni heri awe marehemu yeye kuliko wengine”.