Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, akiwa jijini Arusha ameteketeza Tani 8 za Nyama zilizooza yaani ambazo zilikuwa zimekamatwa kwa makosa ya kuingia nchini bila vibali pia zikiwa zimekwisha muda wa matumizi.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amempongeza Waziri Mpina kwa jitihada alizozifanya za kuhakikisha watu wanafuata Sheria katika Mazao ya Mifugo na Uvuvi.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Bodi ya Nyama, Praygod Lukio amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya Sheria ya Mwaka 2016 kosa la kuingiza bidhaa ambayo imekwisha muda wa matumizi na kuiuza inatajwa kuwa ni kosa la kuhujumu Uchumi, ambapo adhabu yake ni Kifungo cha Miaka 14.

Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli imeamua kupambana na wafanyabiashara wenye nia mbaya ya kuhujumu uchumi wa nchi na kutaka kuwaangamiza Wananchi kiafya kwa kuingiza Mazao ya Mifugo na Uvuvi yaliyopitwa na muda wamatumizi (Expire).