Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Utumishi wa umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman
akizungumza katika Sherehe yaugaaji wa tunzo kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar beach resolte Mazizini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Utumishi wa umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman amewataka Waandishi wa Habari kutumia taaluma zao kwa kukemea masuala ya rushwa yaliopo katika jamii.


Akizungumza katika Sherehe yaUgawaja tunzo kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar beach resolte Mazizini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.


Waziri harouna amesema Waandishi wa habari wanauwezo mkubwa wa kuifikia jamii hivyo Watakapo kemea masuala ya Rushwa watawezaa kuisaidia serikali kufikia malengo yake.


Amesema Rushwa ni janga kubwaa linaloharibu Uchumi na Maendeleo ya Nchi hivyo ni vyema kwa Waandishi wa Habari kuelimisha jamii pamoja na kutowa taarifa kwa taasisi wa zinajihusisha na masuala ya Rushwa.
“Rushwaa ni janga la taifa ambalo linaharibu uchumi na maendeleo ya Nchi,kwa hiyo kilaa mwananchi hususan Waandishi wa habari tusilifumbie macho suala hili”….Alisema Waziri Haroun.


Waziri Haruna pia Ameitaka Mamlaka ya kuzuia Rushwa (ZAECA) kuendelea kufatilia kesi za Rushwa zikizopo katika jamii hususani hususani katika masuala ya ajira yanayowakosesha fursa watu wenye sifa na kuajiriwa.


Amesema mbali na ajira pia ni vyema kufatilia masula ya Rushwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2020 unaotarajiwa hivi karibu.


Amesema kuna kesi nyingi za Rushwa zinajitokeza katika kipindi cha uchaguzi jambo ambalo linawanyima fursa za msingi Wananchi.   Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar Mussa Haji Ali amesema wataendelea kushirikiana na Waandishi wa Habari katika kukemea masuala ya Rushwa katika jamii.   

Amesema Waandishi wa habari wamekuwa chanzo kikubwa cha kupataa taarifaa za rushwa jambo ambalo linaengeza uweledi katika kutekeleza majukumu yao.   

Aidha ametowa wito kwa Wananchi kuendelea kuripoti kesi za Rushwa wanazokutana nazo katika jamii ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.   

Nae Mwakilishi kutoka shirika la umoja wa Mataifa la kupambana na Rushwa na kuia Ugaidi (UNODC)kutoka Kenya Mohamed Jaafar amesema wataendelea  kukemea masula ya Rushwa kupitia miradi wanaoisimamia pamojanna kuwataka waanfishi wa habari kuengeza bidiii katika kupambana na rushwa.   


Mwakilishi kutoka shirika la umoja wa Mataifa la kupambana na Rushwa na kuia Ugaidi (UNODC)kutoka Kenya Mohamed Jaafar
katika Sherehe yaUgawaja tunzo kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar beach resolte Mazizini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Hata hivyoo ametowa wito kwa Zaeca kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za Rushwa pamoja na kuhamasisha jamii kutumia vyema namba za huduma kwa wateja ili waweze kuwasilishwa kesi za Rushwa kwa wakati.   

Tunzo hizo zimetolewa kwa waandishi wa habari Wa vyombo mbalimbali ikiwemo Zanzibar24 tv online,Zanzibar leo Gazeti pamoja na Chuchu fm Radio ambapo imeandaliwa na ZAECA kwa kushirikiana na UNODC ili kuengeza bidii ya kuapambana na Vitendo vya Rushwa Nchini.Na.

Na: Fat-hiya Shehe.